Kutembea njia ya huduma

Ingawa muundo wa kidhana unaoongoza kazi za Taasisi ya Ruhi unashughulikia ukuaji wa kiroho wa mtu binafsi, inatambulika kuwa hali ya kiroho ya mtu na maendeleo yake ni mambo ambayo Mungu peke yake anayeweza kuyahukumu na kwamba wanadamu wasidiriki kuyapima. Taasisi kwa hiyo imechukua njia ya kielimu ambayo inajihusisha yenyewe na mbinu ambazo kwazo watu binafsi wanaweza kusaidiwa kuongeza uwezo wao wa kutoa huduma. Uwezo huu, wakati umeunganika na hali ya kiroho, hufanya kazi kwa uhusiano na hali hiyo katika njia ambazo hazihitaji kuelezwa kinagaubaga. Yatosha kuelewa kuwa nyanja ya huduma huwakilisha mazingira ambamo hali ya kiroho inaweza kulelewa.

Mchakato wa hatua kwa hatua wa elimu ya kiroho huanzishwa pale ambapo watu binafsi wanapo sindikizwa katika njia za huduma ambazo wamechagua kuzifuata, kulingana na mapenzi yao na uwezo wao. Kwa kujenga juu ya tajiriba iliyopatikana kwa kufanya kazi na watu nchini Colombia, Taasisi ya Ruhi imeainisha “njia maalum za huduma”. Uelewa unakuzwa katika kila njia kupitia mfululizo wa kozi, ambazo baadhi yao huingiza stadi na mielekeo inayohitajika kutekeleza vitendo vya huduma, ambapo vingine huwasilisha mafundisho ya kiroho na maagizo ambayo huvipa maana vitendo hivi.


Kama ilivyopendekezwa na yaliyotangulia, mlolongo mkuu wa kozi za Taasisi haujapangiliwa kufuatana na mfululizo wa maudhui ya mada, kwa madhumuni maalum ya kuongeza ujuzi wa mtu binafsi. Maudhui na mpangilio umejikita, hivyo, juu ya mfululizo wa vitendo vya huduma, ambayo utekelezaji wa mara nyingi hujenga uwezo ndani ya mtu binafsi wa kukabiliana na mahitaji ya jumuiya zinazoendelea kukua. Na pia kama ilivyoonwa hapo juu, uimarishaji wa uwezo kama huo unaonwa kama kufuatana na “kutembea njia ya huduma”. Katika njia kama hiyo, watu binafsi wanasaidiwa kwanza katika utimizaji kazi rahisi na kisha kutekeleza kazi zenye utata zaidi na zinazohitaji vitendo vya huduma. Hii ndio asili ya ujengaji wa uwezo: mtu mmoja anakusindikiza kadiri unapokuwa unajifunza kutembea njia hiyo mwenyewe. Uangukapo, yupo mtu karibu wa kukuinua. Makosa yanakubalika. Polepole kujiamini kunajengeka. Uwekaji malengo makubwa sana na kujenga shauku kubwa kupitia sihi za kihisia huepukwa.

Vitendo vya huduma vilivyoshughulikiwa katika mlolongo mkuu wa kozi za Taasisi, kwa hiyo vinakusudia, kusitawisha ruwaza ya nguvu ya utendaji ambayo itapelekea kwenye maendeleo thabiti ya jumuiya za mahali. Ruwaza hii ya utendaji inahusisha uanzishwaji wa mikutano ya ibada, programu ya ziara za nyumbani, madarasa ya watoto, vikundi vya vijana chipukizi na vikundi vya mafunzo—zikiimarishwa na juhudi za mtu binafsi na za pamoja kwa ajili ya kushiriki mafundisho ya Bahá’u’lláh katika mandhari tofauti.

Kwa kuongeza kwa mlolongo wake mkuu, Taasisi ya Ruhi inaendeleza angalau seti mbili za kozi ambazo zimechepuka kutoka humo. Kozi hizi za mchepuo huwaruhusu washiriki kufuata njia maalum zaidi za huduma, wakati wanaendelea na usomaji wao wa mlolongo mkuu wa kozi. Kozi katika seti ya kwanza zitawapa mafunzo wale wanaopenda elimu ya watoto; wale waliomo katika seti ya pili watakuza uwezo wa kufanya kazi na vijana chipukizi.

Maelezo ya zana za kozi zilizomo katika mlolongo kuu, halikadhalika michepuo yake miwili, yametolewa hapo chini. Kwa ujumla, vikundi vidogo vya washiriki, wakifanya kazi kwa msaada wa mkufunzi, hukutana pamoja katika mandhari yenye furaha, tulivu na yenye tafakari kwa ajili ya kujihusisha kwa karibu zaidi ya nyenzo za kozi. Mchakato wa ujengaji wa uwezo ambao unaibuliwa na usomaji wa nyenzo unaibuka kila mahali ulimwenguni unaelezwa na  Nyumba ya Haki ya Ulimwengu kwa maneno haya:

Maelfu kwa maelfu, ikikumbatia tofauti ya familia nzima ya binadamu, wanashiriki  katika kujifunza Neno la Uumbaji kwa utaratibu maalum katika mazingira ambayo papo hapo ni makini na yainuayo. Kadiri wanavyojitahidi kutumia umaizi walioupata kupitia mchakato wa utendaji, tafakari na ushauriano umaizi uliopatika hivyo, wanaona uwezo wao wa kuhudumia Hoja ukipanda hadi kwenye viwango vipya.. . . ”

Ujumbe wa 21 Aprili 2008 kutoka Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Mawazo Juu ya Maisha ya Roho

Kitabu cha 1

Pakua PDF

Kitabu cha kwanza katika mlolongo wa kozi kwa sehemu kubwa kinahusu suala la utambulisho. Ni upi utambulisho halisi wa “Mimi” katika sentensi hii “Mimi ninatembea  njia  ya huduma”? Sura tatu za utambulisho wa mtu binafsi zinachunguzwa katika kitabu: “Uhalisia wa uwepo wangu ni roho yangu ambayo hupitia katika ulimwengu huu kupata sifa inazohitaji kwa ajili ya safari ya milele na iliyotukuka kumwelekea Mungu. Muda wangu ninaouthamini sana ni ule ambao ninautumia katika kuwasiliana na Mungu, kwa sababu sala ni chakula cha kila siku ambacho roho lazima ikipokee kama inahitaji kutekeleza kusudi lake lililotukuka. Mojawapo ya wazo langu kuu kabisa katika maisha haya ni kujifunza Maandiko Matakatifu, kujaribu kuongeza uelewa wangu wa mafundisho matakatifu, na kujifunza kuyatumia katika maisha yangu ya kila siku na kwa maisha ya jumuiya”. Kitabu kinajumuisha vitengo “Ufahamu wa Maandiko ya Kibahá’í”, “Sala”, and “Uhai na Kifo”. Kinawahamasisha wale wanao kisoma kuchukua hatua ya kwanza katika njia ya huduma kwa kukaribisha mkutano wa ibada na kuabudu katika nyumba zao.

Wakiitikia shauku ya ndani kabisa ya kila moyo ya kutaka kuzungumza na Muumba wake, hutekeleza shughuli za ibada ya pamoja katika mazingira mbalimbali, wakiungana na wengine katika sala, wakiamsha hisia za kiroho na kufanya mtindo wa maisha unaobainishwa kwa tabia yake ya ibada.”

21 Apriil 2008 ujumbe kutoka kwa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Uinikaji kwa Kuhudumu

Kitabu cha 2

Pakua PDF

Kitabu cha 2 cha mlolongo mkuu hufikiria juu ya nini humaanisha kutembea  njia  ya huduma. Hujumuisha vitengo vitatu. Cha kwanza kinachunguza asili ya furaha mtu aipatayo kwa kuwahudumia wengine, ambapo vingine viwili vinavyofuata vinalenga zaidi juu ya ujuzi, uwezo na sifa zihitajikazo kuingia katika mazungumzo ambayo yanainua akili na roho. Uwezo wa kuinua mazungumzo ya siku hadi siku kwa kutambulisha kanuni za kiroho, pale tukio linapoidai, imewasilishwa katika kitengo cha pili. Cha tatu, halafu kinageukia kwenye maisha ya jumuiya. Kuwatembelea marafiki na majirani katika majumba yao kujadiliana dhima zilizojikita kwenye uwepo wa kiroho na kijamii – kitendo cha pili cha huduma kinachohamasishwa katika mlolongo mkuu – huimarisha mafundo ya umoja na undugu, muhimu sana kwa maisha ya pamoja. Vitengo hivi vitatu vinaitwa: “Furaha ya Ufundishaji”, “Mazungumzo yenye Kuinua”, na “Mada za Kujiongezea Elimu zaidi”.

Kadiri wanavyotembeleana majumbani mwao mmoja kwa mwingine na kufanya ziara kwa familia, marafiki na jamaa zao huingia katika majadiliano yaliyokusudiwa juu ya mada za umuhimu wa kiroho…na hukaribisha idadi inayoongezeka, kujiunga nao katika shughuli kubwa kabisa ya kiroho.”

21 Aprili 2008 ujumbe kutoka kwa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Kufundisha Madarasa ya Watoto, Daraja la 1

Kitabu cha 3

Pakua PDF

Kitendo cha tatu cha huduma kinacho wasilishwa na Taasisi ya Ruhi kimo katika eneo la elimu ya kiroho ya watoto. Elimu ya watoto ni ya muhimu kwa ajili ya mabadiliko ya jamii. Kitabu cha 3 hulenga juu ya baadhi ya maarifa, ujuzi na sifa zinazohitajika kwa wale wanaotaka kuingia katika uwanja huu muhimu wa huduma. Kinahusisha vitengo viwili, ‘Baadhi ya Kanuni za Elimu ya Kibahá’í’ na ‘Masomo kwa ajili ya Madarasa ya Watoto Daraja la 1.’ Kitengo cha kwanza huchunguza kanuni na dhana fulani zinazopatikana kwenye elimu kutoka mtazamo wa Kibahá’í. Pia hujadili namna mwalimu anavyoweza kusimamia darasa kwa kiwango kikubwa cha upendo na uelewa, kwa wakati huohuo, kuwa na nidhamu inayohitajika kujenga mazingira sahihi ya ujifunzaji. Kitengo cha pili hutoa seti ya masomo ishirini na nne yaliyokusudia kuendeleza maendeleo ya sifa za kiroho katika watoto wadogo – sifa kama unyoofu, ukarimu, na uaminifu. Baadhi ya zana kwa ajili ya maandalizi ya mwalimu zimejumuishwa.

Wakitambua hamu ya watoto wa dunia na mahitaji yao ya elimu ya kiroho, wanaeneza jitihada zao kwa mapana kujumuisha makundi yanayoongezeka daima ya washiriki katika madarasa ambayo yamekuwa ni vituo vinavyovutia kwa ajili ya watoto na kuimarisha mizizi ya Imani katika jamii.”

21 April 2008 ujumbe kutoka kwa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Wadhihirishaji Pacha

Kitabu cha 4

Pakua PDF

Kitabu cha 4 katika mlolongo mkuu hurejea kwenye swali la utambulisho, “Mimi” katika tamko “Mimi ninatembea njia ya huduma”. Historia hubumba sehemu kubwa ya utambulisho wa watu binafsi, hali kadhalika koo nzima ya watu. Kitengo cha pili na cha tatu katika kitabu vimejikita kwenye ujifunzaji wa historia ya maisha ya Bahá’u’lláh, Mtunzi wa Imani ya Kibahá’í, na Mtangulizi Wake, Báb. Katika kitengo cha kwanza, ukuu wa Siku hii umechunguzwa kwa kifupi. Kwa kuona kwa uwazi vipengele vinavyoainisha siku zilizopita, huwawezesha watu binafsi kuchangia zaidi kwa ufanisi katika kubumba mustakabali.

“Wanapokuwa wanatembeleana majumbani mwao, na kutembelea familia, marafiki, na jamaa, [wao] huongeza kina cha ujuzi wao… na kukaribisha idadi inayoendelea kuongezeka ya watu kuungana nao katika kazi hii ya kiroho yenye nguvu.”

21 April 2008 ujumbe kutoka kwa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Uachiliaji wa Uwezo wa Vijana Chipukizi

Kitabu cha 5

Pakua PDF

Kitabu hiki kina nafasi maalum katika mlolongo wa Taasisi ya Ruhi. Kufuatana na mafundisho ya Kibahá’í, mtu binafsi hufikia umri wa ukomavu afikishapo miaka 15, wakati anapo banwa na majukumu ya kimaadili na ya kiroho. Miaka inayotangulia umri huu, kwahiyo, ina umuhimu maalum. Hiki ndicho kipindi ambamo dhana za kimsingi kuhusu maisha ya mtu binafsi na ya pamoja zinaundwa ndani ya akili ya kijana chipukizi anayejitahidi kuacha nyuma tabia za utoto. Vijana wenye rika ya kati ya miaka 12 na 15 wanayo mengi ya kusema, na yeyote anayechukulia kama watoto hupoteza fursa ya kuwasaidia kujenga utambulisho wao sahihi. Vitengo vitatu vinavyokifanya Kitabu cha 5 hulenga juu ya baadhi ya dhana, stadi, sifa na mielekeo ambavyo tajiriba imeonesha vinahitajika kwa wale wanaopenda kutekeleza programu kwa ajili ya uwezeshwaji wa kiroho wa vijana chipukizi.

 “Wao wanawasaidia vijana chipukizi kwa kuwaongoza kupitia kipindi muhimu sana cha maisha yao na kuwezeshwa kuelekeza nguvu zao kwenye uendelezaji wa ustaarabu.

21 April 2008 ujumbe kutoka kwa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Ufundishaji Hoja

Kitabu cha 6

Pakua PDF

Watu kutoka kila usuli wanakaribishwa  kuchunguza mafundosho ya Bahà'u'llàh na kujifunza jinsi wanavyoweza kuyatumia kuboresha maisha yao. Wabahá’í wote, hivyo, hushiriki kwa uhuru na bila masharti mafundisho na maagizo ya Imani yao. Ingawa uenezaji wa ujumbe wa Bahá’u’lláh  ni moja ya huduma muhimu kabisa inayoweza kutolewa, ufundishaji pia ni uwasilishaji asilia wa hali ya kuwa - hali ambamo mtu hushiriki na wengine ujuzi na furaha aipatayo kwenye Ufunuo Wake. Dhana hii inachunguzwa katika kitengo cha kwanza cha Kitabu cha 6, “Asili ya Kiroho ya Ufundishaji”. Huchukulia kama kauli yake uelewa  kwamba “kuwa” na “kutenda” ni nyanja za maisha ya kiroho. Kitengo cha pili na cha tatu “Sifa na Mielekeo Muhimu kwa ajili ya Ufundishaji” na “Kitendo cha Ufundishaji” huichukua kauli hii zaidi. Kitengo cha pili huchukulia namna hali ya ndani ya mtu inavyochangia kwenye, na huimarishwa na, juhudi za mtu katika uga wa huduma, wakati kitengo cha tatu hutazama jinsi kitendo cha Ufundishaji kinavyopaswa kuendewa. Ya muhimu wa kipekee ni mfano uliotolewa katika kitengo cha tatu, kupitia hadithi ya Anna na Emilia wa namna ya kutambulisha Imani kwa mtu anayeifahamu kidogo.

“Kadiri wanavyotembeleana majumbani mwao, na kufanya ziara kwa familia, marafiki, na jamaa, [wao] hugawana ujumbe wa Bahá’u’lláh, na kukaribisha idadi inayoendelea kuongezeka ya watu kuungana nao katika kazi hii ya kiroho yenye nguvu.”

21 April 2008 ujumbe kutoka Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Kutembea Pamoja katika Njia ya Huduma

Kitabu cha 7

Pakua PDF

Kitabu cha 7 kinaongelea kitendo cha huduma muhimu kwenye mchakato wa ujengaji uwezo ulioonwa katika nyenzo za Taasisi ya Ruhi – yaani kusaidia kundi la watu binafsi kusoma kwa ufanyaji kazi wa Taasisi ya Ruhi yenyewe, yaani, kusaidia kundi la watu binafsi kujifunza kozi zake za mlolongo mkuu. Kwamba watu binafsi huambatana mmoja kwa mwingine katika njia ya huduma kwa jumuiya zao ni kiini cha mchakato huu wa ujengaji wa uwezo. Kitengo cha kwanza cha kitabu hiki huchunguza nguvu za kiroho za kuendelea katika njia iliyochorwa na kozi na huinua uelewa wa nguvu zinazofanya kazi. Kitengo cha pili “Kuhudumu kama Mkufunzi wa Kozi za Taasisi,” huchunguza dhana hizo, mielekeo, sifa na ujuzi ambavyo humwezesha mtu binafsi kutekeleza kitendo hiki cha huduma, kwa ujumla kuleta pamoja marafiki nane au kumi kwenye kile kinachoitwa “kikundi cha mafunzo”. Kitengo cha tatu, “Uendelezaji wa Sanaa katika Ngazi ya umma,” kimeundwa kwa ajili ya kuthamini wajibu wa jitihada za kisanii katika kukkuza mchakato wa kielimu uliokuzwa na kozi na katika kuimarisha ruwaza za maisha ya jumuiya ambamo inaibuka.

Maelfu kwa maelfu, ikikumbatia tofauti ya familia nzima ya binadamu, wanashiriki  katika kujifunza Neno la Uumbaji kwa utaratibu maalum katika mazingira ambayo papo hapo ni makini na yainuayo.

21 April 2008 ujumbe kutoka Nyumba ya Haki ya Ulimwengu

Agano la Bahá’u’lláh

Kitabu cha 8 (toleo la kabla ya uchapishaji)

Vitengo ambavyo vitakiunda kitabu hiki kwa sasa vinapatikana katika mfumo wa kabla ya uchapishaji, na maelezo ya maudhui yao yatakuja.

Kupata Mtazamo wa Kihistoria

Kitabu cha 9 (toleo la kabla ya uchapishaji)

Vitengo ambavyo vitakiunda kitabu hiki kwa sasa vinapatikana katika mfumo wa kabla ya uchapishaji, na maelezo ya maudhui yao yatakuja.

Kujenga Jumuiya Hai na Zenye Kupuma

Kitabu cha 10 (toleo la kabla ya uchapishaji)

Vitengo ambavyo vitakiunda kitabu hiki kwa sasa vinapatikana katika mfumo wa kabla ya uchapishaji, na maelezo ya maudhui yao yatakuja.

Nyenzo za Kimwili

Kitabu cha 11 (zana inayoendelezwa)

Vitengo ambavyo vitakiunda kitabu hiki kwa sasa vinapatikana katika mfumo wa kabla ya uchapishaji, na maelezo ya maudhui yao yatakuja.

Familia na Jumuiya

Kitabu cha 12 (zana inayoendelezwa)

Vitengo ambavyo vitakiunda kitabu hiki kwa sasa vinapatikana katika mfumo wa kabla ya uchapishaji, na maelezo ya maudhui yao yatakuja.

Kujihusisha katika Shughuli za Kijamii

Kitabu cha 13 (zana inayoendelezwa)

Vitengo ambavyo vitakiunda kitabu hiki kwa sasa vinapatikana katika mfumo wa kabla ya uchapishaji, na maelezo ya maudhui yao yatakuja.

Kushiriki katika Mjadala wa Umma

Kitabu cha 14 (zana inayoendelezwa)

Vitengo ambavyo vitakiunda kitabu hiki kwa sasa vinapatikana katika mfumo wa kabla ya uchapishaji, na maelezo ya maudhui yao yatakuja.

Kuhusu  mchakato wa ujifunzaji ulioanzishwa na usomaji wa kozi, hususan asili yake shirikishi, mshiriki mmoja wa mwanzo wa Taasisi ya Ruhi ameandika:

. . . sisi ni wajumbe wa jumuiya ambazo zimetawanyika kote ulimwenguni ambazo zinashughulika na kazi kubwa kabisa, ile ya kujenga ustaarabu mpya. Mazungumzo yetu—mazungumzo katika vitendo—kuhusu sura tofauti za kazi hii yanafanyika katika mandhari nyingi: Karamu ya Siku Kumi na Tisa, mikutano ya Mabaraza ya Kiroho na kamati, Shule za Kiangazi, madarasa ya kujiimarisha zaidi, makongamano, miradi ya ufundishaji, jitihada za maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kadhalika. Mlolongo mkuu wa kozi wa taasisi ya mafunzo hutafuta kuweka utaratibu wa hatua kwa hatua kwa sura muhimu ya maongezi yetu ya kidunia yanayohusu maendeleo ya jumuiya ambazo zinajitahidi kutumia mafundisho ya Kibahá’í. Idadi inayoendelea kukua zaidi kila pembe ya sayari inafanya maongezi kama hayo katika mandhari tunayoyaita kundi la mafunzo. Nyenzo tunazojifunza huyaandaa maongezi haya. Huandika kumbukumbu za vipengele muhimu na huhakikisha kwamba mawazo yetu na vitendo vinaangaziwa na aya husika kutoka maandiko ya Imani.

Katika mandhari haya, mkufunzi wa kikundi cha mafunzo anasema kitu kama hiki: “Sisi tunatembea njia ya huduma ambayo inaturuhusu kuchangia kwa maendeleo ya jumuiya zinazotambua sura za kimwili na kiroho za uwepo. Tunafanya hivyo kwa kujifunza, kutenda na kutafakari juu ya utendaji kufuatana na kile tulichojifunza. Zana hizi zimenisaidia kukuza baadhi ya vipaji ninavyohitaji katika kutembea njia hii. Ninaamini zitawasaidieni ninyi pia. Maelfu ya vikundi hivi ulimwenguni vinafanya vivyo hivyo. Vinafanya mazungumzo yale yale, na tajiriba pana inaendelea kujengeka miongoni mwa watu wa kila usuli katika hali tofauti. Kile tutakachofanya kitakuwa sehemu ya tajiriba hii ya kidunia. Kile tunachosema kinatajirisha mazungumzo. Kile tunachojifunza kitawekwa katika utaratibu wa hatua kwa hatua na kusambazwa kati ya jumuiya kote ulimwenguni na asasi ambazo tumesha zisitawisha. Ushiriki wetu katika mchakato huu wa ujifunzaji wa kidunia unaweza kuonwa kwa jinsi hii. Tunashiriki katika mchakato wa ujifunzaji wa kidunia, tukijifunza kujenga uwezo wa jumuiya ya Kibahá’í wa kufungua wazi milango yake kwa watu wa . . .”