Kauli ya kusudi na madhumuni

Taasisi ya Ruhi ni asasi ya kielimu, inayofanya kazi chini ya mwongozo wa  Baraza la Kiroho la Kitaifa la Wabahá’í wa Colombia, ambalo huweka juhudi zake katika maendeleo ya rasilimali watu kwa ajili  ya maendeleo ya kiroho, kijamii, na kitamaduni ya watu wa Colombia. Ingawa makao yake yapo katika mji wa Puerto Tejada katika sekta ya Cauca, eneo lake la ushawishi hufikia nchi nzima. Hasa katika miaka ya hivi karibuni, programu zake za kielimu zimefuatwa na idadi iongezekayo ya mawakala ulimwenguni kote.

Kama asasi yoyote nyingine inayojihusisha kwenye mchakato wa elimu kwa ajili ya maaendeleo, Taasisi ya Ruhi imeunda mikakati yake ndani ya muundo maalum wa kiutendaji na falsafa ya mabadiliko ya kijamii, maendeleo na elimu. Katika suala hili,  uelewa huo umeibuka kutoka juhudi ya kutumia kanuni za Kibahá’í katika uchambuzi wa hali za kijamii.


Imani ya Kibahá’í huona hali ya wakati huu ya msuala ya kibinadamu kama hatua ya kiasilia katika mchakato unaoendelea kukua ambao hatimaye utapelekea kwenye umoja wa mbari ya binadamu1 ndani ya utaratibu wa mmoja wa kijamii. Jamii ya binadamu kwa ujumla imepitia hatua za ukuaji wa hatua kwa hatua zinazofanana na zile zinazopitiwa na mtu binafsi; baada ya kupitia uchanga na utoto, sasa inapitia  nyakati ngumu za kufikia mwisho wa ujana chipukizi.2 Hali ya wakati huu ya kuchanganyikiwa, mashaka, na ukaidi unapaswa kueleweka kama hali za kijana chipukizi ambaye anatamani kwa nguvu ukuaji na ukomaavu, lakini akingali amejiambatanisha  na mielekeo ya kitoto na desturi. Bado muda umewadia  kwa kijana chipukizi huyu kuchukua hatua ya mwisho na kuingia katika hatua inayojenga  na nguvu lakini yenye uzani wa ukomaavu na utu uzima.


Wakati wa kuchambua mabadiliko yanayotokea kwa kasi ulimwenguni leo, Wabahá’í wanabaini michakato  miwili ya sambamba inayofanya kazi kwenye ngazi zote— jamii ya kijiji, mji, taifa, na ya kidunia. Kwa upande mmoja, ni wazi kuwa jamii  ya wanadamu  inateseka  kutokana na mchakato wa mmomonyoko unaojitokeza wakati wa vita, ugaidi,  ghasia, utovu wa usalama wa kimwili na kisaikolojia , hali ilyoenea kila mahali ya umasikini wa kimali. Kwa upande wa pili, nguvu za muungano zinawasogeza watu binafsi na vikundi kuelekea kukubali thamani mpya, mifumo mipya ya mpangilio, na miundombinu inayofaa ambayo inaweza kuweka msingi wa kusitawisha utaratibu mpyawa kijamii. Taasisi ya Ruhi inaeleza kusudi lake la msingi la kuwa kama njia kwa ajili ya nguvu za kiroho za wakati wetu ziweze kutumika  katika maisha ya umati wa  jamii ya wanadamu, kuwaimarisha kuweza kuchangia katika usitawishaji wa ustaarabu mpya wa ulimwengu.


Katika juhudi zake za kuelewa na kuchangia  kwenye mchakato wa mabadiliko ya kijamii, Taasisi ya Ruhi hujaribu kuepuka seti mbili za kinadharia3 ambazo zimetawala mjadala wa maendeleo na mabadiliko kwa kipindi cha miongo mingi. Kwa upande mmoja, haikubaliani na dhana za mabadiliko ya  kijamii ambazo ni  zenye ubinafsi katika muonekano wao,4 ambazo zinaichambua jamii tu kufuatana na muumbo wa kisaikolojia, stadi,  na tabia za mtu binafsi, na ambazo zinachukulia kuwa  miundo ya kijamii kwa namna fulani  zitabadilika zenyewe pindi mtu akikombolewa au akifunzwa vizuri kupitia mazungumzo ya kidini au elimu ya kidunia. Kwa upande mwingine, pia hukataa nadharia ambazo zinazomchukulia binadamu kwa ujumla kama matokeo ya jamii , na kudai kuwa  maboresho hayawezekani kabisa, mpaka miundo ya kijamii, hasa yale yanayohusiana na nguvu ya siasa na kiuchumi,5 zinabadilishwa kwanza. Kuna mifano mingi ya ushiriki inayofanywa na “waadilifu” na “waliofunzwa vyema” katika miundo ya udhalimu ili kuruhusu mtazamaji yeyote makini  wa michakato  ya kijamii nzima kukubali  mapendekezo ya mabadiliko ambayo yanawekwa kabisa juu ya misingi ya  wokovu  ya mtu binafsi bila umakini kwa nguvu na miundo ya kijamii. Kwa wakati huo huo, historia tayari imeonesha uovu wa mifumo inayokanusha uhuru wa mtu binafsi  na hujitwalia kanuni zao za kimaadili na kijamii kutoka mtazamo wa ulazima wa mabadiliko katika miundo ya uwezo, mabadiliko ambayo watetezi wake wanaamini yanapaswa kupatikana kwa gharama yoyote.

Taasisi ya Ruhi hujaribu kuelewa mchakato wa mabadiliko ya jamii  ya binadamu kulingana na seti yenye utata mkubwa zaidi  wa mwingiliano wa utendaji kati ya mifumo miwili inayoenda sambamba ya maendeleo: mmbadiliko wa mtu binafsi, na uumbaji wa makusudi wa miundo ya jamii mpya. Aidha, kama vile isivyowatazama binadamu kama matokeo tu ya mwingiliano wa utendaji wa asili na jamii, ndivyo isivyo baini mabadiliko ya miundo kuwa michakato ya kisiasa na kiuchumi. Bali, inaona ulazima wa mabadiliko katika miundo yote—kiakili, kitamaduni, kisayansi na kiteknolojia, kielimu, kiuchumi na kijamii—ikijumuisha mabadiliko kamili katika kila dhana ya uongozi wa kisiasa na nguvu. Inaeleweka kuwa  watu binafsi, ambao wote wanamiliki sana au kidogo asili ya kiroho iliyoendelea, wanaweza kuangazwa na mafundisho matakatifu, hata katika ushawishi wa nguvu za kijamii zenye dhulma kabisa. Watu hawa kwa hiyo, ambao hawajakamilika kabisa, hujaribu kutembea njia ya mabadiliko ya kijamii, njia ambayo, kwa vyovyote, siyo ya wokovu wa mtu binafsi bali ambayo inaashiria juhudi endelevu ya kuumba na kuimarisha mashirika ya utaratibu mpya wa kijamii. Mashirika haya mapya, hata yanapokuwa yameundwa kikamilifu, pengine hayawezi kufanya kazi kikamilifu hapo mwanzoni, lakini yanaiwezesha idadi kubwa ya watu kutembea mbele zaidi katika njia ya ukuaji wa kiroho na mabadiliko. Mwingiliano huu endelevu, kati ya michakato  sambamba ya kukuza roho ya mtu binafsi na usitawishaji  wa miundo mipya ya kijamii, inaeleza njia pekee inayoweza kutegemewa ya mabadiliko ya kijamii, ile inayoepukana na yote mawili majigambo na ukali na isiyoendeleza duru ya udhalimu na uhuru wa uwongo ambao jamii ya binadamu imepitia katika nyakati zilizopita. Kufuatana na muono huu wa mabadiliko ya kijamii, Taasisi ya Ruhi huelekeza juhudi zake za wakati huu kwa ajili ya kukuza rasilimali watu ndani ya seti ya shughuli ambayo ni bora kwa ukuaji wa kiroho na wa akili, lakini  zinafanyika katika muktadha wa mchango wa kila mtu binafsi kuanzisha miundo mipya, iwe vijijini na kanda za vijijini au katika vituo vya miji mikubwa.


Bado kipengele kingine muhimu cha muundo wa kinadharia wa Taasisi ya Ruhi ni dhana ya ushiriki.6 Ingawa hadi sasa programu nyingi zinazohusika na maendeleo na mabadiliko hukubali umuhimu wa ushiriki wa jumuiya ya mahali katika njia yake yenyewe ya kuepuka kuweka miradi yao wenyewe na mawazo, mara nyingi upo uwazi mdogo na makubaliano  kuhusu asili, umbo na ukubwa wa ushiriki huu. Taasisi ya Ruhi, ikifuata mawazo yaliyowasilishwa katika aya zilizotangulia, hudai kwamba ushiriki wenye ufanisi ambao hautatokea kwenye udanganyifu wa kisiasa  huhitaji mchakato wa hatua kwa hatua wa ujifunzaj ndani ya kila jumuiya na kanda7 ili jumuiya yenyewe iweze kufanya majaribio kwa kutumia mawazo mapya, mbinu mpya, na teknolojia na taratibu mpya badala ya kuwa kitu cha kufanyiwa majaribio ya kijamii ya wengine. Hivyo, mojawapo ya hatua za mwanzoni ni ustawishaji wa michakato  shirikishi ya maendeleo katika kanda, ni kuendeleza ushiriki shadidi wa idadi inayoendelea kuongezeka  ya  watu binafsi katika kujifunza, katika juhudi inayoendelea wakati wote ya kutumia ujuzi kwa ajili ya kuboresha  hali za  maisha ya jumuiya na kuumba na kuzipa nguvu asasi za utaratibu mpya wa ulimwengu.


Kwa kuongozwa na ushiriki wa wote, vyote kama kanuni na pia kama lengo, Taasisi ya Ruhi inajaribu kutengeneza na kutekeleza shughuli za kielimu  ambazo zinachanganya ujifunzaji wa darasani na wa mtu binafsi pamoja na vitendo vya huduma ndani ya jumuiya. Kila shughuli ya kielimu inahitaji kuwa, yenyewe binafsi, tajiriba inayowezesha ambayo husaidia washiriki kukuza uelewa, sifa, mielekeo, uwezo, na ujuzi wa aina mpya ya wahusika wa kijamii ambao nguvu zao zote zinaelekezwa kuelekea uendelezaji wa ustawi wa jumuiya, na ambao vitendo vyao vinahamasishwa na muono wa ustaarabu mpya wa ulimwengu ambao utabeba katika miundo yake yote na michakato ya kanuni ya kimsingi ya umoja wa mbari ya binadamu.


Kwenye  Taasisi ya Ruhi , muundo na utekelezaji wa shughuli za kielimu  daima huongozwa na imani ya kina kabisa ya juu ya asili ya msingi ya ubora wa binadamu.8 Maandiko ya Kibahá’í husema:

Mtu ni Talisimu  Kuu kabisa. Ukosefu wa elimu inayofaa umekuwa, hata hivyo, kumnyima kile anachomilki kiasili. Kupitia neno litokalo kinywani mwa Mungu yeye  aliletwa katika uwepo; kwa neno moja lingine moja  zaidi aliongozwa kutambua Chanzo cha elimu yake; na kwa neno lingine bado daraja lake na hatima yake vililindwa. Yule Mkuu Aliyepo husema: Mfikirie mtu kama machimbo la madini lililojaa vito vya thamani isiyokadirika. Elimu pekee yaweza kufichua hazina zake, na kumwezesha binadamu kunufaika kutoka humo.9

Elimu, basi, haionwi tu kama upataji wa ujuzi na ukuzaji wa stadi, lakini pia  kufuatana na  ukuzaji wa uwezo mpana na  nguvu kubwa sana vilirithiwavyo kiasili ndani ya kila binadamu. Tena, ukuzaji wa  uwezo na vipaji, ambavyo vinachukuliwa ni haki na wajibu wa mtu binafsi alivyopewa na  Mungu, hupata matunda pale vinapofuatwa kwa roho ya huduma kwa jamii ya binadamu na katika muktadha wa kuumba ustaarabu mpya wa ulimwengu.

Kila mshiriki katika programu za taasisi ya Ruhi hudenda kama mwanafunzi katika shughuli fulani za kielimu, na ni mkufunzi kwa nyingine. Taasisi, kwa hiyo, hutumia msamiati “mshiriki” kuwarejelea wote wanaoshiriki katika program zake. Juu ya msingi wa hali na mahitaji ya umma unaohudumiwa na taasisi, kozi zinaandaliwa katika mfululizo wa  “njia za huduma” ambazo mshiriki hufuata kufuatana na mapenzi yake binafsi na uwezo wake. Mwanzoni mwa kila njia ya huduma washiriki kwa sehemu kubwa hujifunza na kukuza dhana mapya na stadi. Baadaye, hushiriki katika kozi ambazo huwaandaa kufanya kazi kama wakufunzi wa kozi za mwanzoni, na hivyo kuumba mazingira ya kipekee na endelevu kwa ajili ya ukuzaji wa rasilimali watu.

Viungo vya nje  vya nyaraka zifuatazo vimo katika maandiko yaliyopo hapo juu:

Prosperity of Humankind [Ustawi wa Jamii ya Binadamu]. Tamko lililotayarishwa na Ofisi ya Habari ya Jumuiya ya Kimataifa ya Kibahá’í ambayo inajadili juu ya asili ya utajiri wa kidunia.

Promoting a Discourse on Science, Religion and Development [Kuendeleza  Mjadala juu ya Sayansi, Dini na Maendeleo]. Andiko lililotayarishwa na Farzam Arbab, mfizikia na mwanzilishi wa FUNDAEC.

Science, Religion and Development: Some Initial Considerations [Sayansi, Dini na Maendeleo: Baadhi ya Fikra za Mwanzo]. Tamko lililotayarishwa na  Taasisi kwa ajili ya Masomo katika Ustawi wa Ulimwengu, asasi iliyojikita  kuweka utaratibu wa hatua kwa hatua  wa ujuzi uliozalishwa na watu binafsi na mashirika yanayoendeleza ustawi na usalama wa watu wa ulimwengu.

Maelezo

  1. Tazama pia: Promoting a Discourse on Science, Religion and Development, “The oneness of humankind” [Uendelezaji wa Mjadala juu ya Sayansi, Dini na Maendeleo, “Umoja wa jamii ya binadamu”], ukurasa 198; Prosperity of Humankind [Ustawi wa Jamii ya binadamu], Sehemu ya I

  2. Tazama pia: Promoting a Discourse on Science, Religion and Development, “Spiritual Principles and the Role of Knowledge” [Uendelezaji wa Mjadala juu ya Sayansi, Dini na Maendeleo, “Kanuni za Kiroho na Jukumu la Ujuzi”], ukurasa 196

  3. Tazama pia: Promoting a Discourse on Science, Religion and Development, “The Direction of Development” [Uendelezaji wa Mjadala juu ya Sayansi, Dini na Maendeleo, “Mwelekeo wa Maendeleo”], ukurasa 161; kama hapo juu., “The state and the market” [“Nchi na soko”], ukurasa 174

  4. Tazama pia: Promoting a Discourse on Science, Religion and Development, “Freedom and empowerment” [Uendelezaji wa Mjadala juu ya Sayansi, Dini na Maendeleo, “Uhuru na uwezeshaji”], ukurasa 204

  5. Tazama pia: Promoting a Discourse on Science, Religion and Development, “Power and Authority” [Uendelezaji wa Mjadala juu ya Sayansi, Dini na Maendeleo, “Uwezo na Mamlaka”], ukurasa 211; Prosperity of Humankind [Ustawi wa Jamii ya binadamu], Sehemu ya VI

  6. Tazama pia: Science, Religion and Development: Some Initial Considerations, “Historical Background” [Sayansi, Dini na Maendeleo: Baadhi ya mazingatio ya Mwanzoni, “Usuli wa Kihistoria”], ukurasa 3

  7. Tazama pia: Promoting a Discourse on Science, Religion and Development, “The Role of Knowledge” [Uendelezaji wa Mjadala juu ya Sayansi, Dini na Maendeleo, “Wajibu wa Ujuzi”], ukurasa 205; kama hapo juu., “Decision-Making and Implementation” [“Ufanyaji Maamuzi na Utekelezaji”], ukurasa 213

  8. Tazama pia: Promoting a Discourse on Science, Religion and Development, “Nobility” [Uendelezaji wa Mjadala kwa ajili ya Sayansi, Dini na Maendeleo, “Ubora”], ukurasa 175

  9. Tablets of Bahá’u’lláh Revealed after the Kitáb-i-Aqdas, Lawḥ-i-Maqṣúd (Tablet of Maqṣúd) [Nyaraka za Bahá’u’lláh Zilizofunulliwa baada ya Kitáb-i-Aqdas, Lawḥ-i-Maqṣúd (Waraka wa Maqṣúd)]