Maendeleo ya mtaala

Mbinu iliyofuatwa na Taasisi ya Ruhi ya kukuza mtaala siyo kwa kawaida ya kuunda, kujaribu ugani na kutathmini, inayofanywa kwa mtiririko wa mfuatano. Bali hatua ya kwanza katika kuandika seti yoyote ya zana inachukuliwa, pale ambapo tajiriba  fulani inapozaliwa kwenye ngazi ya umma katika utekelezaji wa huduma inayoitikia wito wa mahitaji ya maendeleo ya jumuiya moja. Zana hizi huibuka kutokana na tajiriba hii na zinakuwa vielelezo vyake. Kuna, kwa upande mmoja, kumbukumbu ya ujifunzaji ambao hutokea katika kutumia mafundisho ya Imani katika eneo maalum la huduma na, kwa upande mwingine,  chombo kwa ajili ya kuweka kiutaratibu ujifunzaji huo. Mbinu imekwisha elezewa katika istilahi zifuatazo katika juzuu ndogo iitwayo Kujifunza Kuhusu Ukuaji:

Pindi hitaji la kielimu linapobainika, kikundi kidogo cha watu, wanaofanya kazi kwenye ngazi ya umma, hushauriana miongoni mwao wenyewe, hukuza seti ya mawazo kwa ajili ya shughuli za kielimu, na kuyatekeleza. Matokeo ya zoezi hili hupitiwa upya, hutathminiwa na hujadiliwa; katika mwanga wa ushauriano huu, seti ya shughuli za kielimu iliyoboreshwa hufanyiwa mazoezi, na hufanyiwa tafakari ambayo hupelekea kwenye marekebisho zaidi na marudio. Hakuna wakati wowote katika mchakato huu wa kukuza mtaala ambamo utekelezaji hungojea matayarisho ya mwisho na tathmini ya zana za kielimu. Katika kila hatua, shughuli za kielimu huendelea kwa zana bora zilizopo mikononi, kwa kuamini kuwa ni kupitia mazoezi na tafakari peke yake, yote mawili yakifuatiliwa kufuatana na Ufunuo wa Bahá’u’lláh, kwamba mitaala inayofaa taratibu inaweza kukuzwa. Bado, hii siyo mandhari ambamo watu wachache tu wanakuza zana kwa ajili ya matumizi yao wenyewe, na hufika wakati ambapo ni lazima kukamilisha muundo na maudhui ya kila kitengo ili kiweze kutumika kwa uhakika na watu wengine. Uamuzi wa kuachilia toleo la mwisho la zana kwa ajili ya kozi yoyote ile hufanywa pale ambapo inapogundulika kwamba mahitaji ya maboresho yamekuwa kidogo. Ni muhimu kutambua kwamba vipengele mbalimbali vya mchakato wa ushauriano, utendaji, na tafakari hufanyika sambamba kwa moja na nyingine, na haufanyiki kwa mfuatano wa mlolongo ambao ungekuwa bandia kiasili.

Katika utekelezaji mbinu ya hapo juu huchukua hali tofauti, kufuatana na asili ya zana inayoendelea  kukuzwa. Kwa ujumla, hata hivyo, baadhi ya hatua tatu zinaweza kubainiwa katika mchakato wa ukuzaji, ambao hupelekea kile kinachodhahaniwa kuwa toleo la mwisho lililochapishwa.

  1. Muhtasari wa Mwanzo
    Kwenye hatua hii kozi au kitabu hubeba dhana za kimsingi na seti ya aya kutoka maandiko ya Kibahá’í ambayo, yakichukuliwa kwa pamoja, huaminiwa kufanikisha lengo la kielimu linaloongelewa. Kwa kipindi fulani, muhutasari huu wa mwanzo wa mawazo hutumiwa na vikundi vidogo vya watu binafsi ugani,  kama sehemu ya juhudi za kuelezea maudhui yenye ufanisi ya  kozi.

  2. Toleo la kwanza
    Kadri utendaji unavyoendelea, zana zinaboreshwa na huanza kuakisi tajiriba mpya iliyopatikana, kuingiza mawazo ambayo yanaibuka kutokana nao. Siyo nadra, kuwa baadhi ya mawazo hurekebishwa, aya mpya za maandiko ya Kibahá’í huongezwa, au mlolongo wa mazoezi rahisi hutambulishwa ili  kurahisisha uelewa wa mada au kusaidia kukuza ustadi muhimu au mwelekeo. Kupitia mchakato huu, kozi iliyounganishwa au kitabu huibuka ambacho kwa jumla hujulikana kama “toleo la kwanza”.

  3. Toleo la Kabla ya Uchapishaji
    Katika wakati inaamuriwa, kwa ujumla  juu ya msingi wa hadhi wa maudhui, kuifanya kozi au maandiko kupatikana kwa upana zaidi kama toleo la kabla ya uchapishaji. Kupitia matumizi yake yanayoendelea kutumika, inakuwa dhahiri pale  sehemu inahitaji kusogezwa au zoezi moja au lingine linahitaji kurudiwa upya. Matoleo kadhaa yanayofuatana yanaweza kutokea. Pole pole, hata hivyo, marekebisho machache na machache Zaidi yanahitajika kufanikisha kusudi lililokusudiwa la kozi au maandiko, na nyenzo, katika hatua hii, hupelekwa kwa ajili ya kuchapisha.