Vijitabu vya historia

Mara nyingi wale wanaokutana na mafundisho ya Bahá’u’lláh na kujifahamisha na nguvu yake ya mabadiliko katika maisha yao wamevutiwa katika kujifunza zaidi kuhusu Utu wake na hali za kihistoria ambazo zilipelekea kutokea kwa Imani ya Kibahá’í. Vijitabu hapo chini vinatoa uwasilisho rahisi wa maisha Yake na maisha ya mtangulizi Wake, Báb. Huu unaweza kutumika kufungua mazungumzo kuhusu umuhimu wa kipindi hiki cha kihistoria, wakati Walielimishaji wawili wapya wa ulimwengu wamekuja kuongoza jamii ya binadamu na kuisaidia kusogea kwenye hatua mpya ya maendeleo. Kwa wale wote wanaohitaji kwenda mbele zaidi, kozi ya nne katika mlolongo wetu mkuu, Wadhihirishaji Pacha, hutoa maelezo ya maisha yao kwa kina.