Wabahá’í kila mahali wanajihusisha katika mchakato wa ulimwengu wa kujifunza ambao unawasaidia kujenga uwezo wao wa kutumia mafundisho ya Bahá’u’lláh kwenye mbadiliko wa jamii. Kama mchango kwenye mchakato huu wa kujifunza, taasisi ya Ruhi hutekeleza utendaji na utafiti ugani, ili kuendeleza programu na nyenzo ambazo zinakuza uwezo wa watu binafsi na jumuiya kwa ajili ya kuhudumia jamii ya wanadamu. Kukuza uwezo katika mtu binafsi unaweza kufananishwa na kutembea katika njia ya huduma, kama ilivyoelezwa katika nukuu za hapo chini kutoka ujumbe wa Nyumba ya Haki ya Ulimwengu, chombo chenye mamlaka ya kimataifa cha Imani ya Kibahá’í.

Katika tovuti hii tunatoa baadhi ya taarifa kuhusu programu zetu, pamoja na hali za kihistoria na nadharia ya ufundishaji iliyopo kwenye msingi wa maendeleo yao. Kwa wale wote ambao, wanajali mustakabali wa wanadamu, wanatamani uboreshaji wa ulimwengu, tunaviweka vitabu saba vya kwanza katika mlolongo wetu mkuu wa kozi. Wote wanakaribishwa kuvisoma na kujadili maudhui yao pamoja na marafiki wachache.

Taasisi ya Ruhi
28 Februari 2024

Mlolongo mkuu wa kozi za Taasisi ya Ruhi unaandaliwa kwa namna ambayo itamwezesha mtu binafsi. . .

“. . . katika njia ambayo imeelezwa kwa uzoefu wa jumuiya unaoendelea kukusanywa katika jitihada zake kufungua kwa binadamu maono ya utaratibu wa Ulimwengu wa Bahá’u’lláh.”

“Wazo lenyewe la njia, ni ishara ya asili na makusudi ya kozi, kwani njia hukaribisha ushiriki,huashiria peo mpya,hudai jitihada na mjongeo, huruhusu hatua na tambo mbali mbali, ina muundo na mipaka.”

“Njia inaweza kuzoeleka na kufahamika, siyo na mtu mmoja au wawili bali makorija kwa makorija; inamilikiwa na jumuiya.”

“Kuitembea njia ni dhana ambayo ni sawa na msemo unaojieleza. Huhitaji uchaguzi na hiari ya mtu binafsi; huhitaji seti ya ujuzi na uwezo lakini pia huvutia sifa fulani na mielekeo; hulazimisha maendeleo yenye mantiki lakini hukubali, inapohitajika,njia husika za uchunguzi; inaweza kuonekana rahisi mwanzoni lakini inakuwa na changamoto zaidi inavyoendelea mbele.”

“Na cha muhimu, mtu hutembea kwenye njia akiwa pamoja na wengine.”